DUNIA MAPITO
Kuna familia ya mjomba wangu imeishia pabaya sana. Najitahidi kuamini vinginevyo lakini akili yangu inaniambia ni laana. Mjomba wangu alikuwa ni msomi wa Ph.D na alikuwa na pesa kama uchafu. Majumba, magari na miradi mingine kibao. Alikuwa na mke na watoto watano wa kike wawili na wa kiume watatu. Watoto wote walikuwa wamesoma shule za maana, namaanisha za maana sio za umma ila shule za maana za kimataifa ambazo hata watoto wa mabwenyenye wangesoma bila shida. Vyuo baadhi yao wamesoma nchi za ng'ambo. Mjomba alikuwa ni mtu mwenye upendo na alisaidia sana ndugu zake. Kiukweli alikuwa ni mtu ambaye ametoboa sana kimaisha ukilinganisha na ndugu zake wengine wa ukoo mzima. Baadaye aliugua afya yake ikazorota sana na akili zikawa kama zimeruka kidogo (sio sana). Mkewe na watoto wake hawakumjali. Kila alilowaambia hawakumsikiliza akawa hana thamani tena. Huwezi amini mfanyakazi wa kiume wa nyumbani alimtunza na kumjali kuliko mkewe na kizazi chake. Kuna siku wa...