MGAO WA MALI
Kesi ya Mirathi ilipelekwa mahakamani huko Voi.
Kijana wa miaka 20 alikuwa anataka kupewa mgao wake wa mali za marehemu baba yake.
Ni kweli alikuwa na mgao wake, ila mjane wa marehemu, ambaye ni mama yake mzazi, alikuwa anamuona bado mdogo kuweza kumiliki mali nyingi kiasi kile.
Marehemu alikuwa ameacha magari na nyumba kadhaa.
Basi yule kijana baada ya kuona mama yake hataki kumpa mgao wake akafungua kesi Mahakamani.
Kufika mahakamani Hakimu akamuuliza yule kijana:
"Unamtambua huyu Mwanamke?"
Kijana Akajibu: "Ndiyo. Ni Mama yangu Mzazi."
Na mama akaulizwa, "Unamtambua Huyu Kijana?"
Mama akajibu,: "Ndio ni Mwanangu wa Kumzaa."
Hakimu akamuuliza yule Kijana: "Kijana, Eleza Mahakama Madai Yako ni Yepi?"
Kijana akajibu: "Madai yangu nina taka nikabidhiwe mgao wangu wa mali za marehemu baba. Ila Mama nimemwambia amegoma kunipa."
Mama akaulizwa na Hakimu: "Unasemaje Kuhusu Haya Madai ya huyu Kijana!?"
Mama akajibu: "Huyu ni Mwanangu wa Kumzaa, ila Sikumzaa na Huyo Aliyeacha Hizo Mali."
Kesi ikaishia hapo hapo...π₯π₯π₯Kina Mama wakiamua wanawezaπ♂️
Comments
Post a Comment